Michezo

French Open kupamba moto,ni Laura Robinson dhidi ya Caroline Wozniack

Mwanadada raia wa Uingereza na mcheza Tennis nambari moja Laura Robson anatarajia kumkabili bingwa wa zamani wa mchezo huo Caroline Wozniacki katika mzunguko wa awali wa michuano ya French Open huku bingwa wa zamani Wozniacki akielekea mtanange huo akiwa ameshapoteza karibia mizunguko minne ya awali.

Caroline Wozniack anatarajia kuumana na Laura Robinson katika michuano ya French Open
Caroline Wozniack anatarajia kuumana na Laura Robinson katika michuano ya French Open AFP
Matangazo ya kibiashara

Muingereza nambari mbili Heather Watson atakabiliana na Stefanie Voegele,huku hali kiwa tete kati ya Elena Baltacha na Marina Erakovic.

Kukoseakana kwa Bingwa Andy Murray kufuatia majeraha yanayomsumbua inamaanisha hakutakuwa na mtanange kati ya wanaume waingereza kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1994.

Rafael Nadal anaelekea katika taji la nane la michuano ya French open ambako kutamkutanisha na bingwa nambari moja Novak Djokovic katika nusu fainali baada ya kutoka sare.

Awali Nadal atamkabili mjerumani Daniel Brands wakati Djokovic akikutana na mbelgiji David Goffin.

Bingwa mtetezi Maria Sharapova atauanza mchezo dhidi ya Su-Wei Hsieh wa Taipei,China.