FORMULAR ONE

Bodi inayosimamia mashindano ya mbio za magari ya F1 kuichunguza kampuni ya Mercedez

gari la kampuni ya Mercedez ambayo itachunguzwa iwapo walijaribu tairi zake kinyume cha sheria
gari la kampuni ya Mercedez ambayo itachunguzwa iwapo walijaribu tairi zake kinyume cha sheria Reuters

Bodi ya shirikisho linalosimamia mashindano ya mbio za magari yaendayo kasi zaidi duniani Langalanga ama Formular one imetangaza kuanzisha uchunguzi rasmi kuhusu tuhuma dhidi ya kampuni ya Mercedez kuhusu kujaribu matairi mapya kinyume cha sheria.

Matangazo ya kibiashara

Tuhuma dhidi ya kampuni ya Mercedez zimetolewa na viongozi wa Red Bull na Ferrari ambao wanadai kuwa kwa siku tatu mfululizo kampuni ya Mercedez imekuwa ikishiriki kwenye majaribio ya matairi mpaya kinyume cha sheria.

Tuhuma hizo zimetolewa mara baada ya kumalizika kwa mbio za Monaco Grand Prix ambapo kampuni ya Mercedez iliibuka na ushindi kupitia dereva wake Nico Roseberg ambapo inadaiwa kuwa kamouni ya matairi ya Pirelli ilitumia kampuni hoyo kufanyia majaribio tairi zake ambapo kisheria hairuhusi kufanya hivo wakati wa msimu.

Taarifa iliyotolewa na bodi ya FIA imesema kuwa inafikiri kuliwasilisha suala hilo mbele ya mahakama inayosimamia mchezo huo na kwamba hatua zaidi zitachukuliwa iwapo ikibainika ni kweli kampuni ya Mercedez imefanya hivyo.

Kwenye mbio hizo, dereva wa kamouni ya Mercedez, Nico Roseberg alimaliza wa kwanza akifuatiwa na Sebastian Vettel na Mark Webber toka kampuni ya Red Bull huku nafasi ya nne ikishikwa na Lewis hamilton wa Mercedez na nafasi ya tano ikishikwa na Adrian Sutil wa kampuni ya Force India.