MPIRA WA MIGUU - SANTOS - FC BARCELONA

FC Barcelona yamnasa Neymar da Silva kutoka klabu ya Santos ya Brazil

Mchezaji, Neymar da Silva Santos Junior ambaye atajiunga na klabu ya FC Barcelona msimu ujao akitokea kalbu ya Santos
Mchezaji, Neymar da Silva Santos Junior ambaye atajiunga na klabu ya FC Barcelona msimu ujao akitokea kalbu ya Santos Reuters

Klabu ya FC Barcelona ya Uhispania hatimaye imefikia makubaliano na mchezaji anayekipiga na kalbu ya Santos ya Brazil, Neymar da Silva Santos Junior kujiunga na klabu hiyo kwenye msimu ujao wa ligi. 

Matangazo ya kibiashara

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anatarajiwa kumaliza mazungumzo na klabu ya Barcelona ambapo atatia saini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo.

Hapo jana mchezaji huyo kupitia mtandao wa Instagram aliandika kuwashukuru mashabiki wa klabu ya Santos kwa kumuunga mkono kwa karibu miaka tisa yote aliyokuwepo klabuni hapo na sasa anaenda kucheza soka barani Ulaya.

Mtandao wa klabu ya FC Barcolena uliandika kuwa "unayofuraha kutangaza kufanikiwa kumsajili mshambuliaji wa timu ya Santos Neymer kwa mmkataba wa miaka mitano na ni furaha kubwa kwa kabu kufanikisha hilo".

Neymer amekuwa akiwindwa na vlabu kadhaa barani Ulaya ikiwemo klabu ya Manchester City na Chelsea ambazo zilitenga dau kubwa kuweza kumsajili mshambuliaji huyo bila mafanikio.

Hata hivyo klabu ya Barcelona haijaweka wazi dau waliloafikiana na klabu ya Santos na kudai kuwa itaweka wazi mara baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati yao.

Wachambuzi wa masuala ya michezo wanamtaja Neymer kama mmoja wa washambuliaji chipukizi ambaye kipaji chake kinaelezwa kukua kadri muda unavyozidi kwenda.