FRENCH OPEN

Venus Williams atupwa nje kwenye michuano ya tenesi, French Open

Michuano ya Tenesi ya French Open inayofanyika jijini Paris Ufaransa imeendelea kushika kasi huku ikushuhudiwa baadhi ya magwiji wa mchezo huo wakitolewa kwenye hatua za awali.

Venus Williams
Venus Williams Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa michuano hiyo hii leo ikiingia siku yake ya tatu, hapo jana zimeshuhudiwa mechi kadhaa ambapo mwanadada Venus William alijikuta akipoteza mechi yake ya kwanza kwa kukubali kufungwa na Urszula Radwanska kwa seti mbili kwa moja kwa matokeo ya 7-6, 6-7 na 6-4.

Katika mechi nyingine mdogo wa Venus, Serena Williams yeye amefanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya kuchomoza na ushindi dhidi ya Anna tatishvill kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 6-0 na 6-1.

Mechi nyingine ilimkutanisha Anastasia Pavlyuchenkova alipambana na Andrea Hlavackova kwenye mchezo ambao Anastasia alifanikiwa kuchomoza na ushindi wa seti mbili kwa moja kwa matokeo ya 4-6, 7-4 na 6-4.

Kwa upande wa wanaume mchezaji David Ferrer alifanikiwa kuchomoza na ushindi dhidi ya mpinzani wake Marinko Matosevic kwa seti tatu bila kwa matokeo ya 6-4, 6-3 na 6-4 na kusonga mbele.

Kwa upande wake mchezaji nambari mbili kwa ubora wa mchezo huo, Roger Federer alifanikiwa kusonga mbele kwa kumfunga Pablo Carreno kwa seti tatu bila, kwa matokeo ya 6-2, 6-2 na 6-3.