MPIRA WA MIGUU - UINGEREZA

Crystal Palace yarejea kushiriki ligi kuu ya Uingereza msimu ujao

Mkongwe Kevin Phillips jana jioni alipeleka furaha kwa mashabiki wa timu ya Crystal Palace baada ya kuipatia timu yake bao la ushindi na kuicusha kushiriki ligi kuu ya Uingereza msimu ujao.

Wachezaji wa Crystal Palace wakipongezana baada ya kufuzu kucheza ligi kuu ya Uingereza msimu ujao
Wachezaji wa Crystal Palace wakipongezana baada ya kufuzu kucheza ligi kuu ya Uingereza msimu ujao Reuters
Matangazo ya kibiashara

The 39-year-old, a loser in three previous play-off finals, struck from the penalty spot at the end of the first half of extra time as the Eagles ended an eight-year absence from the Premier League.

Mchezo huo ambao ulipigwa katika dimba la Wimbley uliamuliwa ndani ya muda wa dakika za nyongeza ambapo wakati mpira ukikaribia kumalizika, Crystal Palace walizwadiwa penalt ambayo iliwekwa kimiani na mkongwe Phillips.

Penalt hiyo ilitolewa baada ya beki wa Watford Marco Cassetti kumfanyia madhambi mchezaji Wilfried Zaha ambaye msimu ujao atakuwa anaitumikia klabu ya Manchester United.

Wakati mchezo huo ukikaribia kumalizika almanusura, Watford wasawazishe bao lakini mpira wa kichwa uliopigwa na Joel Ward uliokolewa kwenye mstari na mlinda mlango wa Palace, Fernando Forestieri.

Timu ya palace ilinusurika kushuka daraja kwenye msimu wa 2009-10 baada ya kukabiliwa na ukata ambao ungeilazimu timu hiyo kushushwa daraja kabla ya kufanikiwa kujikomboa na sasa kurejea kwenye ligi kuu ya Uingereza.