FRENCH OPEN

Nadal aponea chupuchupu kutolewa kwenye michuano ya French Open

Michuano ya tenesi ya French Open imeendelea kushika kasi huku baadhi ya magwiji wa mchezo huo wakiponea chupuchupu kuondoshwa kwenye michuano hiyo na wachezaji chipukizi.

Mchezaji Rafael Nadal akipiga mpira wakati wa mechi yake hiyo jana
Mchezaji Rafael Nadal akipiga mpira wakati wa mechi yake hiyo jana Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hiyo jana mchezaji nambari tatu kwa ubora wa mchezo huo, Rafael Nadal, alijikuta kwenye wakati mgumu wa kusonga mbele kufuatia upinzani alioupata toka kwa Daniel Brands, mchezo ambao uliishia kwa Nadal kuibuka na ushindi wa 4-6, 7-6, 6-4 na 6-3.

Katika mchezo mwingine, Gael Monfils alifanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya kufanikiwa kuchomoza na ushindi dhidi ya Tomas Berdych kwa ushindi wa seti tatu kwa mbili.

Mfaransa, Jo-Wilfried Tsonga yeye alifanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Aljaz Bedene kwa seti tatu kwa bila kwa matokeo ya 6-2, 6-2 na 6-3.

Kwa upande wa wanawake, mchezaji Caroline Wozniack alifanikiwa kusonga mbele baada ya kumfunga Laura Robson kwa seti mbili kwa bila kwa matokeo ya 6-3 na 6-2.

Kwa upande wake Agnieszka Radwanska yeye amefanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa seti mbili kwa bila kwa matokeo ya 6-1 na 6-1 dhidi ya Shahar Peer.