UINGEREZA

Cole kuwa nahodha wa Uingereza mechi ya kirafiki na Ireland hii leo, Kolo Toure asajiliwa na Liverpool

Beki wa kushoto wa Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza, Ashley Cole ambaye atakuwa nahodha kwenye mechi ya kirafiki hii leo dhidi ya Ireland
Beki wa kushoto wa Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza, Ashley Cole ambaye atakuwa nahodha kwenye mechi ya kirafiki hii leo dhidi ya Ireland Reuters

Beki wa kushoto wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza, Ashley Cole ametangazwa kuwa nahoha ya timu yake ya taifa wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Ireland.

Matangazo ya kibiashara

Mechi ya leo inamfanya Cole kuwa moja kati ya wachezaji ambao wamecheza mechi nyingi zaidi wakiwa na timu ya taifa ambapo atafikisha mechi yake ya mia moja na timu ya taifa ya Uingereza.

Kocha Roy Hodgoson akizungumza na waandishi wa habari kabla ya mechi yao itakayopigwa hii leo, amesema Cole atakuwa nahodha wa mechi ya leo na kwamba Steven Gerrads ataendelea kubakia kama nahodha mkuu akisaidiwa na Frank Lampard.

Hodgson ameongeza kuwa Cole amekuwa na mchango mkubwa sio tu kwa kalbu ya Arsenal na Chelsea lakini amekuwa mchango mkubwa kwa timu ya taifa ya Uingereza kutokana na umahiri wake.

Katika masuala ya usajili nchini Uingereza, klabu ya Liverpool imefanikiwa kumnasa beki wa kati wa klabu ya Manchester City Kolo Toure kwa dau ambalo mpaka sasa halijawekwa wazi.

Kolo atafanya vipimo juma hili kabla ya kutua rasmi kwenye klabu hoyo July mosi mwaka huu tayari kuanza kutumikia kandarasi yake.

Toure amecheza mechi 102 akiwa na Man Cit toka aliponunuliwa akitokea Arsenal kwa dau la paundi za Uingereza milioni 14.