FRENCH OPEN

Roger Federer, Serena Williams waendelea kutamba michuano ya French Open

Roger Federer
Roger Federer Reuters

Michuano ya tennesi ya french Open inayotimua vumbi jijini Monaco Ufaransa imeendelea kushika kasi huku kwa upande wa wanaume wachezaji magwiji wakiendelea kutamba.

Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa wanaume hiyo jana jioni, mchezaji nambari mbili kwa ubora Riger Federer alifanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya kumfunga, Somdev Devvarman kwa seti tatu bila kwa matokeo ya 6-2, 6-1 na 6-1.

Katika mechi nyingine Marin Cilic alifanikiwa kutinga kwenye hatua inayofuata ya michuano hiyo baada ya kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa seti tatu kwa bila dhidi ya Nick Kyrgios kwa matokeo ya 6-4, 6-2 na 6-2.

Mchezaji nambari sita kwa ubora wa mchezo huo, Jo-Wilfried Tsonga alifanikiwa kutinga kwenye hatua inayofuata baada ya kuchomoza na ushindi wa seti tatu kwa bila dhidi ya Jarkko Roger-Vasselin kwa matokeo ya 7-6, 6-4 na 6-3.

Nicolas Almagro ambaye anashika nafasi ya kumi na moja alisonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya kumfunga Edouard Roger kwa seti tatu bila.

Baadae hii leo rafael Nadal atakuwa na kibarua dhidi ya Martin Klizan.

Kwa upande wa wanawake, mchezaji Na li alifanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya kumfunga Bethanie Mattek-Sands kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 7-5 na 3-1.

Jelena Jankovic yeye alifanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya kufanikiwa kumfunga Gabrine Muguruza kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 6-3 na 6-0.

Mchezaji Samantha Stosur alifanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya kuchomoza na ushindi wa seti mbili bila dhidi ya Kristina Mladenovic kwa matokeo ya 6-4 na 3-1.

Baadae hii leo Eugenie Bouchard atakuwa na kibarua dhidi ya mchezaji nambari mbili kwa mchezo huo, Maria Sharapova wakati  Marion Bartoli atakuwa na kibarua dhidi ya 
Mariana Duque.