SOKA

Mourinho awasili Chelsea kwa furaha kubwa

Jose Mourinho amerejea katika klabu yake ya zamani ya Chelsea akiwa na tabasamu na furaha kubwa na kusema jina lake la utani limebadilika kutoka 'Special One' hadi 'Happy One'.

Matangazo ya kibiashara

Mourinho ambaye kabla ya kurejea kwake katika klabu ya Chelsea alikuwa mkufunzi wa Real Madrid ya Uhispania, amewaambia waandishi wa habari katika uwanja wa Stamford Bridge kuwa anafuraha kubwa kureja nyumbani baada ya miaka tisa ya kuwa nje.

Kocha huyo ambaye pia amewahi kuifunza Real Madrid na Inter Milan wakati mmoja, amesema kuwa yeye ni yule yule na hajabadilika kwa vyovyote vile na anaipenda Chelsea.

Raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 50 mara ya kwanza kuwa kocha wa Chelsea ilikuwa ni kati ya mwaka 2004 hadi 2007  na alipoondoka baada ya kutofautiana na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich.

Mourinho ameongeza kuwa amerudi katika klabu yake ya zamani kwa sababu ya uhusiano mzuri na mmiliki wake Abramovich.

Wakati akiifunza Chelsea kwa mara ya kwanza Mourihno aliisaidia timu hiyo kushinda mataji mawili ya klabu bora nchini humo pamoja na taji la FA.

Chelsea imempa mkataba wa miaka minne.