Michezo-guardiola

Kocha mpya wa Bayern Josep Guardiola aahidi kuendeleza heshma yake ya kuendeleza ubingwa katika klabu yake hiyo mpya

Josep Guardiola kocha mpya wa Bayern Munich
Josep Guardiola kocha mpya wa Bayern Munich

Kocha wa zamani wa Barcelona ya Uhispania Josep Guardiola ambaye amejiunga hivi karibuni na klabu ya Bayern ya nchini Ujerumani ameahidi kuendelea kujilindia heshima yake baada ya kukabidhiwa mikoba ya Jupp Heynckes ya kuinoa klabu hiyo ya Bayern Munich iliobeba vikombe vitatu mfululizo.

Matangazo ya kibiashara

Guardiola amesema unapokuwa kocha unapata shinikizo kubwa, na akiwa hapo shinikizo zinaendelea zaidi, na kwamba anaendela kutanzua changamoto bila tatizo. Guardiola mwenye umri wa miaka 42 ameyasema hayo kwa mara ya kwanza kukutana na vyombo vya habari tangu pale alipo tangazwa kusaini mkataba wa kukinoa kikosi hicho Januari 16 mwaka huu.

Guardiola amesema atafanya marekebisho kidogo kwenye na kuacha kiwango ambacho tayari kimefikia na klabu hiyo, na kwamba atajiweka sawa kwa asilimia mia moja na wachezaji, huku akisema kwamba wachezaji wa Barcelona ni tofauti na wa Bayern licha ya mfumo wa kucheza.

Kocha huyo mpya wa Bayern aliwasili hivi majuzi nchini Ujerumani akitokea New York Marekani na familia yake baada ya mapumziko ya mwaka mmoja, na hivyo kuzungumza na vyombo vya habari akiwa pamoja na viongozi wapya wa klabu hiyo Karl Heinz Rummenigge na Uli Hoeness pamoja na mkurugenzi wa michezo Matthias Sammer.

Akizungumza na vyombo vya habari, Guardiola alianza kuomba radhi kwa matamshi yake ya lugha ya kujerumani ambapo amesema alikuwa nchini Marekani kwa muda wa mwaka mmoja na haikuwa rahisi kwake kujifunza lugha hiyo huko, na baadae aliendelea na mzungumzo katika lugha ya kitaliana.