Michezo-ancelotti-laurent Blanc

Laurent Blanc apewa mkataba wa miaka miwili kuinoa PSG, Carlos Ancelotti apewa mikoba ya Jose Morinho kuinoa Real Madrid

Laurent Blanc kocha mpya wa PSG na Carlo Ancellotti kocha mpya wa Real Madrid
Laurent Blanc kocha mpya wa PSG na Carlo Ancellotti kocha mpya wa Real Madrid Yahoo

Klabu ya Paris Saint Germain ya nchini Ufaransa imemuidhinisha kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo mchezaji na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa le Blue, Laurent Blanc, kwa mkataba wa miaka miwili kuchukuwa nafasi ya Carlo Ancelotti ambaye naye pia ameidhinishwa kuwa kocha mkuu wa Real Madrid ya huko Uhispania kubeba mikoba ilioachwa na Jose Morinho alieelekea nchini Uingereza kuinoa Klabu yake ya zamani ya Chelsea.

Matangazo ya kibiashara

Klabu za Paris Saint Germain ya Ufaransa na Real Madrid ya Uhispania zimetangaza makocha wao wapya baada ya uvumi wa muda mrefu na hivo kusitisha uvumi huo.

Laurent Blanc ameteuliwa kuinoa Paris Germain kwa kipindi cha miaka miwili, nafasi ilioachwa na Carlo ancelotti ambaye amepewa nafasi ya kuinoa Real Madrid kwa kipindi cha miaka mitatu, nafasi ilioachwa na Jose Morinho alieelekea nchini Uingereza kuchukuwa mikoba ya klabu yake ya zamani ya Chelsea the blues.

Carlo Ancelotti atatamublishwa rqasmi kesho mbele ya mashabiki, huku kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa Laurent Blanc akitaraji kutambulishwa katika siku zijazo kama ilivyo fahamishwa katika taarifa iliotolewa na Klabu ya Paris Saint Germain.

Taarifa hizi zimesitisha mbio za muda mrefu katika klabu ya PSG iliokuwa mbioni kumsaka kocha mwenye uwezo wa kuiwezesha klabu hiyo iliochukuwa nafasi ya kwanza katika msimu uliopita kuendelea kutetea taji lake. hii ni baada ya aliekuwa kocha wa Klabu hiyo Carlo Ancelotti kuonyesha nia ya kuondoka katika Klabu hiyo

Hatuwa ya kumkabidhi kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa Mikoba ya Ancelotti imefikiwa mwishoni mwa Juma lililopita.