Brazili

Brazili yailaza Uhispania 3-0 Kombe la Mabara

Mchezaji wa Brazil Neymar akinyanyua juu kombe baada ya kuishinda Uhispania 3-0
Mchezaji wa Brazil Neymar akinyanyua juu kombe baada ya kuishinda Uhispania 3-0 indianexpress.com

Timu ya taifa ya Brazili imeibuka na ushindi mnono dhidi ya Uhispania baada ya kuichakaza kwa magoli matatu kwa nunge katika fainali za kombe la mabara, mtanange uliotimua vumbi katika dimba la Maracana mjini Rio de Janeiro . 

Matangazo ya kibiashara

Timu hiyo ya Brazili tayari inaonyesha ishara kuwa inaweza kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka ujao 2014 itakayofanyika nchini humo.

Timu ya Uhispania ambayo ni mabingwa wa Ulaya imemaliza mechi hiyo ikiwa na wachezaji kumi na mmoja baada mchezaji Gerard Pique kuondolewa dakika ya (68) kwa kosa la kumchezea mchezaji Neymar vibaya.

Kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari amesema kuwa kimsingi matokeo ni mazuri na ni muhimu kuendeleza ndoto ya kuwa mabingwa wa dunia lakini pia alielzea shukrani zake kwa mashiki wa timu hiyo na mshikamano wa wabrazili anaoutaka uwe endelevu.