KENYA

Leopards kumenyana na Thika hii leo bila Abdikaadir na Khamati

Kikosi cha AFC Leopards
Kikosi cha AFC Leopards kenyapage.net

Vinara wa Ligi Kuu ya Kenya, AFC Leopards watawakosa wachezaji wao wapya, kiungo Sadiq Abdikaadir na mshambuliaji Michael Khamati katika mechi yao dhidi ya Thika United . 

Matangazo ya kibiashara

Thika United watamenyana na AFC Leopards leo Jumatatu katika michuano ya Ligi kuu ya Kenya mchezo utakaotimua vumbi kwenye Uwanja wa Nyayo ambapo kocha wa Leopards Mbelgiji Luc Eymael amethibitisha kutokuwepo kwa wachezaji hao wawili kwa sababu za kutowasilishwa mapema kwa stakabadhi zao za usajili ili kupata idhini ya kucheza.

Timu hiyo haijapokea rasmi stakabadhi ya uhamisho kutoka kilabu cha Somalia, Elman FC ambacho Abdikaadir aliechezea huku barua ya kumruhusu Khamati kuhamia timu hiyo kutoka maskani yake ya zamani, Administration Police, haikuwa imewasilishwa kufikia Ijumaa jioni.

Aidha kwa upande mwingine Eymael amethibitisha kuwepo kwa Abdallah Juma na Peter Opiyo ambao wamepewa idhini ya kuichezea Leopards na watajumuishwa katika kikosi chake kitakacho menyana na Thika.