michezo

Serena aondolewa mashindano ya Wimbledon

Bingwa namba moja wa tennis Serena Williams
Bingwa namba moja wa tennis Serena Williams Reuters/Gonzalo Fuentes

Mcheza Tennis Sabine Lisicki raia wa Ujerumani amewashangaza wapenzi wa mchezo huo baada ya kutamatisha rekodi ya ubingwa ya mwanadada Serena Williams ambaye amekuwa bingwa wa mashindano ya Wimbledon kwa miaka kadhaa sasa baada ya kushinda kwa seti tatu za 6-2, 1-6, 6-4 kwenye mzunguko wa nne leo Jumatatu. 

Matangazo ya kibiashara

Lisicki, ambaye alifuzu kutinga kwenye nusu fainali za mashindano ya Wimbledon mwaka 2011, atapambana na Kaia Kanepi kutoka Estonia kuwania kufuzu nusu fainali.

Aidha kwa upande wa wanaume bingwa namba nne mhispania David Ferrer amefanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali kwa mwaka wapili huku Jerzy Janowicz na Lukasz Kubot wakijipanga kwa ajili ya kuwania hatua ya nusu fainali.

Ferrer amemshinda Ivan Dodig kutoka Croatia na kisha atapambana na bingwa namba nane kutoka Argentina Juan Martin del Potro ama Andreas Seppi,bingwa namba 23 kutoka Italia.