KENYA

Ulinzi Stars yapania ushindi dhidi ya Ufaransa

Kikosi cha timu ya soka ya Kenya Ulinzi Stars
Kikosi cha timu ya soka ya Kenya Ulinzi Stars twitter.com

Timu ya Ligi Kuu Kenya Ulinzi Stars imejiandaa vema na iko tayari kukabiliana na Ufaransa katika mechi yao ya ufunguzi katika kinyanganyiro cha Kombe la Dunia la Majeshi leo Jumanne huko Baku, Azerbaijan. 

Matangazo ya kibiashara

Mwalimu wa timu hiyo, Salim Ali amesema kuwa kutokana na maandalizi waliyofanya wamedhamiria kuwashinda wapinzani wao ili kuwapa motisha ya kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza.

Timu hiyo imesafiri na Jumla ya wachezaji 18 wakiwemo Francis Ochieng, James Saruni na mlinda mlango Francis Onyiso huku ngome yao ikilindwa vema na Kelvin Ouma, Josiah Okello, Oliver Kipruto, Mohammed Hassan, James Mulinge na Geoffrey Kokoyo.

Aidha Sambamba na hao Lawrence Owino, Stephen Ochollah, Erick Apul, Kelvin Simiyu, Chester Okoyo, Salim Mohammed wanacheza nafasi ya viungoi wa kati.

Timu za Kenya na Ufaransa zimo katika kundi B pamoja na Bahrain na Algeria.