GHANA-DRC

Mchezaji wa kimataifa wa Ghana Boateng aeleza sababu za kukimbilia DRC

RFI

Mchezaji wa kimataifa wa Ghana Richard Kissi Boateng hatimaye amefunguka na kusema uamuzi wake wa kujiunga na Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ulitokana na hitaji la kupata changamoto mpya katika mchezo wa soka.

Matangazo ya kibiashara

Mchezaji huyo ameechezea kwa kipindi kirefu timu ya Berekum Chelsea kwenye ligi kuu ya Ghana hatimaye alikubali kujiunga na TP Mazembe ili kufanikisha malengo yange katika soka.

Amesema mchezaji anapaswa kuwa wazi juu ya uamuzi anaofanya na sababubu ya yeye kumfanya aondoke kwenye klabu moja na kwenda klabu nyingine na mchezaji wa soka lazima akabailiane na changamoto mpya.

Mchezaji huyo ambaye alikuwa katika timu ya taifa ya Ghana katika fainali za mwisho za Kombe la Mataifa ya Afrika zilizofanyika Afrika Kusini alihamia TP Mazembe mwezi Januari mwaka huu lakini alikuwa hajaeleza sababu za kufanya hivyo.

Richard Kissi Boateng ameongeza kusema kuwa pamoja na sababu hiyo pia alitaka kuipima misuli yakr ili ajue ana uwezo gani katika soka na namna ambavyo anaweza akaendeleza uwezo wake wa soka na kuboresha maisha yake.