HISPANIA

Real Madrid yanasa kinda mpya, yampa mkataba wa miaka mitano

Klabu ya Real Madrid ya Hispania imemtambulisha mchezaji wake mpya wa kiungo Francisco 'Isco' Alarcon mbele ya mashabaiki wao na vyombo vya habari.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo la kumtambulisha mchezaji huyo limefanyika katika uwanja wa Santiago Bernabeu na kushudiwa na mashabiki wa klabu hiyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amesaini mkataba wa miaka mitano kukipiga katika klabu hiyo baada ya kukamilisha taratibu za uhamisho kutoka klabu ya Malaga.

Isco amesema kuwa amefurahi kuwa katika klabu hiyo ambayo anaona kuwa ni bora zaidi na kuongeza kuwa hakuna klabu bora kama Real Madrid.

Francisco 'Isco' Alarcon aliisaidia klabu ya Malaga kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita ikiwa ni pamoja na kuisaidia timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 21ya Hispania.