UINGEREZA

Ryan Giggs ateuliwa kuwa kocha mchezaji Manchester United

RFI

Kiungo wa kati wa Manchester United Ryan Giggs ameteuliwa kuwa kocha mchezaji wa wa timu hiyo, taarifa ambayo imethibitishwa na Klabu hiyo leo Alhamisi. 

Matangazo ya kibiashara

Giggs, mwenye umri wa miaka 39, alitia saini mkataba wa nyongeza wa mwaka mmoja kuendelea kuichezea timu hiyo mnamo mwezi Machi mwaka huu.

Kwa sasa Giggs atajumuisha majukumu yake mapya ya ukocha na kuwa mchezaji katika kikosi cha kwanza.

Meneja wa klabu hiyo David Moyes amesema kuwa amefurahishwa na hatua ya Giggs kukubali nafasi hiyo ya kocha mchezaji.

Kocha huyo ameongeza kusema kuwa fani yake ni mfano kwa mchezaji yeyote anayechipukia na kwamba Giggs na wachezaji wengine watanufaika na na nafasi hiyo mpya.