UFARANSA -TOUR DE FRANCE

Mkimbiza baiskeli wa Ubelgiji Van den Broeck ajiondoa kwenye mashindano ya Tour De France

RFI

Mkimbiza baiskeli wa Ubelgiji Van den Broeck (Lotto), ambaye alitarajiwa kushiriki mbio za tour De France hadi mwisho, amejiondoa katika mbio hizo za baiskeli.

Matangazo ya kibiashara

Van den Broeck amelazimika kujiondoa katika mashindano hayo kabla ya kuingia katika hatua ya sita ya mbio hizo leo Alhamisi kutokana na maumivu.

Timu yake imethibitisha kwamba Van den Broeck hatoshiriki hatua ya sita kutoka Ashien hadi Montpellier kutokana na maumivu ya goti aliyoyapata baada ya kuanguka wakati wa mbio hapo jana .

Van mwenye umri wa miaka 30 amewahi kushika nafasi ya nne katika mbio hizo mara mbili mwaka 2010 na mwaka 2012