NIGERIA

Wizara ya Michezo Nigeria yaunda kamati kuchunguza mgogoro ndani ya Timu ya Super Eagles

Timu ya Nigeria ikichuana na Tahiti nchini Brazili
Timu ya Nigeria ikichuana na Tahiti nchini Brazili REUTERS

Wizara ya michezo nchini Nigeria imeunda kamati ya watu sita kuchunguza mgogoro uliozuka baina ya wachezaji wa timu ya taifa ya soka kuhusu kutolipwa marupurupu yao kabla ya kushsiriki katika michuano ya mabara nchini Brazil mwezi uliopita.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Michezo Bolaji Abdullahi ametangaza kuwa miongoni mwa wale wakaokuwa katika kamati hiyo ni pamoja na mchezaji wa kimataifa wa zamani Garba Lawal na kuongozwa na aliyekuwa mshauri wa rais Segun Adeniyi.
 

Kamati hiyo itanza kazi yake siku ya Alhamisi ikiwa na lengo la kubaini chanzo cha mgogoro huo baina ya wachezaji na kutoa mapendekezo ya kuepeuka kutokea kwa hali kama hiyo katika siku zijazo miongoni mwa wachezaji wa timu ya taifa.
 

Wizara ya michezo imesema kuwa baada ya kamati hiyo kuzinduliwa rasmi itakuwa na wiki mbili kuwasilisha ripoti yake ili kuanza kufanyiwa kazi.
 

Wachezaji wa Super Eagles wamekuwa wakilalamika kuwa wamekuwa hawalipwi marupurupu yao kama wanavyoahidiwa na Chama cha Soka suala ambalo limesababisha baadhi ya kususia michuano ya kimataifa na hata kusabisha matokeo mabaya katika mashindano ya kimataifa.
 

Wakati huo huo Chama cha soka nchini humo NFF kimetangaza Super Eagles itamenyana na Bafana Bafana ya Afrika Kusini tarehe 14 mwezi wa Agosti jijini Durban kwa maandalizi ya michuano ya mwisho kufuzu kwa kombe la dunia nchini Brazil mwaka ujao.
 

Mwenyekiti wa NFF Aminu Maigari amesema kuwa ichuano huo utataumiwa kuonesha heshima kwa rais wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela ambaye anaendelea kupata nafuu.