USAJILI ULAYA

Beyern Munich yaipiku Man utd kuwania saini ya kiungo wa Uhispania, Thiago Alcantara toka Barcelona

Kocha, Pep Guardiola wakati akiwa FC Barcelona akimpa maelekezo kiungo Thiago Alcantara ambaye sasa ataungana nae tena katika klabu ya Beyern Munich ya Ujerumani
Kocha, Pep Guardiola wakati akiwa FC Barcelona akimpa maelekezo kiungo Thiago Alcantara ambaye sasa ataungana nae tena katika klabu ya Beyern Munich ya Ujerumani Reuters

Klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani imeipiku klabu ya Manchester United ya Uingereza katika kuwania saini ya mchezaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Uhispania, Thiago Alcantara.

Matangazo ya kibiashara

Bayern Munich imefanikiwa kukubaliana na FC Barcelona katika kunasa saini ya kiungo huyo kwa dau la paundi za Uingereza milioni 21.6 na sasa atajiunga na kocha wake wa zamani, Pep Guardiola.

Awali Alcantara alikuwa akihusishwa kutaka kujiunga na klabu ya Manchester United ambayo hata hivyo haikuweka wazi iwapo ilikuwa na nia ya dhati ya kumnasa kiuongo huyo aliyewika na Uhispania katika michuano ya kombe la mabara iliyomalizika mwezi huu nchini Brazil.

Pep Guardiola wakati akijiunga na timu ya Bayern Munich alitangaza nia yake ya kutaka kuungana tena na kiungo Alcantara ambaye alimnoa pia kwenye klabu yake ya zamani ya FC Barcelona.

Uongozi wa klabu hiyo umdhibitisha kumnasa mchezaji huyo na kwamba atafanya vipimo vya afya mjini Munich juma lijalo kabla ya kujiunga rasmi na mapingwa hao wa Ulaya na Ujerumani.