MPIRA WA MIGUU

Man utd yatangaza dau la paundi milioni 24 kumnasa kiungo wa Barcelona, Cesc Fabregas

Kiungo wa FC Barcelona, Cesc Fabregas anaetakiwa na klabu ya Man utd
Kiungo wa FC Barcelona, Cesc Fabregas anaetakiwa na klabu ya Man utd REUTERS/Gustau Nacarino

Klabu ya Mancheter United imetangaza dau la paundi milioni 25 kumnasa kiungo wa zamani wa Arsenal na sasa anakipiga na FC Barcelona ya Uhispania, Cesc Fabregas. Dau la mashetani wekundu wa jiji la Manchester linaelezwa kujadiliwa na klabu ya FC Barcelona lakini inafahamika kwamba dau hilo ni dogo ukilinganisha na sera ya Barcelona kwenye kuuza wachezaji wake.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya Frabegas mwenyewe kutolazimisha kuuzwa na kalbu yake lakini mara kadhaa amenukuliwa akisema anegfurahi tena iwapo angerejea kucheza ligi kuu ya Uingereza.

Uamuzi iwapo Barcelona watamuuza mchezaji huyo au la bado uko mikononi mwa viongozi wa timu hiyo ambao wataamua iwapo wanahitaji huduma za mchezaji huyo ama kukubali dau la Manchester United.

Fabregas alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kutegemewa kwenye klabu ya Arsenal chini ya kocha Arsene Wenger lakini aliamua kuikacha klabu hiyo na kujiunga na mabingwa hao wa Uhispania.

Mwaka 2011 mchezaji huyo alitia saini mkataba wa kuitumikia klabu ya Barcelona kwa dau la paundi milioni 25 akitokea Arsenal.

Hii ni mara ya pili kwa Mnachester United kutaka mchezaji kutoka FC Barcelona ambapo ni juma hili tu walishindwa kunasa saini ya kiungo Thiago Alcantara anaejiunga na FC Beyern Munich.

However, he returned to the Nou Camp when he signed a five-year deal with Barcelona in a £25.4m move in August 2011.