RIADHA

Mwanariadha, Yohane Blake atangaza kutoshiriki mashindano ya dunia ya mjini Moscow, Urusi

Mwanariadha wa Jamaica, Yohane Blake.
Mwanariadha wa Jamaica, Yohane Blake. REUTERS/Dylan Martinez

Mwanariadha nguli wa mbio za mita 100 raia wa Jamaica, Yohane Blake ametangaza kutoshiriki mashindano ya dunia yatakayofanyika mjini Moscow Urusi mwezi August mwaka huu kutokana na kuumia. Blake ambaye hakushiriki mashindano ya awali ya kuchagua wachezaji watakaoenda kushirikia michuano hiyo kutokana na kuuguza jeraha lake la mguu, sasa madaktari wanaomtibu nao wamdhibitisha mwanariadha huyo kutoshiriki.

Matangazo ya kibiashara

Yohane Blake alijinyakulia medali kwenye mashindano ya mwaka 2011 mjini dauegu China ambapo mwanariadha mwenzake Usain Bolt hakumaliza mbio hizo kutokana na kukosea kuanza mbio hizo.

Mwanariadha mwenzake wa Jamaica Asafa Powell na mmarekani Tayson Gay nao pia hawatoshiriki maandamano hayo kutokana na kubainika kutumia dawa za kusisimua misuli kwenye mashindano ya mwezi May mwaka huu.

Blake ambaye hakupaswa kushiriki mbio za kufuzu za mita 100 angeingia moja kwa moja kwenye kinyang'anyiro hicho lakini angelazimika kushiriki mbio za kufuzu za mita 100.

Afrika Mashariki yenyewe imepata pigo baada ya mwanariadha wa Kenya, David Rudisha ambaye ni bingwa wa mita 800 wa dunia kutangaza kutoshiriki mashindano haya ya dunia kutokana na kuuguza jeraha la mguu.