MPIRA WA MIGUU-USAJILI-FIFA

Negredo asaini Manchester City, bosi wa FIFA ataka fainali za kombe la duniani la mwaka 2022 zifanyike majira ya baridi

Mshambuliaji mpya wa Man City, Alvaro Negredo
Mshambuliaji mpya wa Man City, Alvaro Negredo Reuters

Klabu ya Manchester City ya nchini Uingereza hatimaye imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji wa klabu ya Uhispania Sevilla, Alvaro Negredo na anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya muda wowote kuanzia sasa. 

Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni mshambuliaji wa pembeni, Jesus Navas alitia saini kuitumikia hiyo kwa mkataba wa paundi milioni 14.9 kwa mkataba wa miaka minne ambapo sasa ataungana na mwenzake Negredo.

Manchester City kwasasa iko ziarani barani Afrika ambapo inapiga kambi nchini Afrika Kusini kwa mechi za kirafiki.

Katika hatua nyingine, rais wa shirikisho la kabumbu duniani FIFA, Sepp Blatter amesema anafikiria uwezekano wa kubadilisha ratoba ya kombe la dunia ili lifanyike wakati wa baridi.

Blatter amesema kwasasa anaandaa muswada wa kuwasilisha kwenye kamati kuu kutaka suala hilo lijadiliwe ili kuangalia uwezekano wa kuhamisha fainali za kombe la dunia za mwaka 2022 ili zichezwe wakati wa baridi.

Blatter anasema kuwa majira ya joto ambayo fainali hizo zitafanyika nchini Qatar, joto litakuwa limefikia kiasi cha centigrade 50.

Ameongeza kuwa licha ya nchi ya Qatar kusema kuwa itatumia air condition kwenye viwanja vyake lakini haitaweza kufanya hivyo baada ya watu kutoka nje ya uwanja kwa hivyo ni lazima kufanyike mabadiliko.