MANDELA-MICHEZO

Wanamichezo duniani wakumbuka siku ya kuzaliwa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela

Nelson Mandela rais wa zamani wa Afrika Kusini
Nelson Mandela rais wa zamani wa Afrika Kusini Reuters

Wanamichezo mbalimbali duniani hii leo wanaadhimisha siku ya kuzaliwa rais wa zamani wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela ambaye alikuwa mshabiki mkubwa wa michezo.

Matangazo ya kibiashara

Nchini Afrika Kusini hii leo kutakuwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa mpira wa miguu kati ya Amazulu FC ya Afrika Kusini na Mnachester City ya Uingereza ambayo ilialikwa nchini humo kwa ziara ya kimichezo.

Baadhi ya wachezaji wa Manchester City wamemwelezea mzee Mandela kama moja ya viongozi ambao walitoa kipaumbele kwa michezo na ndio maana nchi kama Afrika Kusini imepiga hatua kwenye michezo.

Mcheza tennesi Roger Federer na Serena Williams kwa upande wao wamemuelezea Mandela kama mtu aliekuwa anajali wanamichezo na kwamba wakati mmoja wakiwa nchini Afrika Kusini walipata fursa ya kukutana na kiongozi huyo.

Mbali na Afrika Kusini hii leo shughuli mbalimbali za kimichezo zitafanyika duniani kote kuadhimisha siku hii muhimu kwa mzee Mandela ambaye anatimiza umri wa miaka tisini na tano.