SOKA

Uganda Cranes na Taifa Stars kutegua kitendawili cha nani kati yao kutinga fainali za CHAN 2014

www.supersport.com

Jumamosi hii timu ya Uganda Cranes wanakuwa wenyeji wa timu ya soka ya Tanzania “Taifa Stars” katika mchuano wa marudiano ili kusaka tiketi ya kufuzu kwenye fainali za CHAN zitakazotimua vumbi nchini Afrika Kusini hapo mwakani.

Matangazo ya kibiashara

Kocha wa Stars Kim Poulsen amekiri kuwa huenda mechi hii itakuwa ngumu lakini lolote linaweza kutokea katika dakika 90 watakazokuwa ulingoni kwani wao wamefanya maandalizi ya kutosha kabla ya kuelekea.

Naye kocha wa Cranes Micho Sredojevic, amesema wamejiandaa vyema kuhakikisha wanafanya vizuri katika dimba la Nelson Mandela, Namboole nje kidogo ya jiji la Kampala.

Stars inashuka dimbani ikiwa nyuma kwa bao 1-0 walilopachikwa katika mechi ya awali iliyopigwa Julai 13 jijini Dar es salaam na wanahitaji ushindi wa mabao 2-0 au zaidi ili wafanikiwe kutinga katika fainali hizo.