SOKA

Golikipa wa Liverpool Jose Reina ailaumu klabu yake kumlazimisha kujiunga na Napoli ya Italia

premiershipticketsonline.com

Golikipa wa klabu ya soka ya Liverpool Jose Reina amesema hajafurahishwa na uamuzi wa klabu yake kumlazimisha kujinga na klabu ya Napoli ya Italia kwa msimu mmoja, Reina anaishutumu Liverpool kufikia maamuzi hayo bila kumshirikisha.

Matangazo ya kibiashara

Liverpool ilikubali Reina aende akaichezee kwa mkopo Napoli baada ya kocha Brendan Rodgers kumsajili Golikipa Simon Mignolet wa nchini Sunderland.

Reina alijiunga na Liverpool mwaka 2005 na mkataba wake utamalizika mwaka 2016, lakini kwa maelezo yake mwenyewe alipenda zaidi kusakata kabumbu katika klabu ya Barcelona kuliko alikopelekwa hivi sasa.

Hapo awali kulikuwa na taarifa kuwa Reina mwenye umri wa miaka 30 angejiunga na klabu ya Barcelona ya nchini Uhispania hata hivyo suala hilo halikufanikiwa.

Reina kwa mara nyingine anakutana na Kocha Rafael Benitez ambaye awali alikuwa akikinoa kikosi cha Liverpool.