SOKA

Manchester United yasema haitamuachia mshambuliaji wake Wayne Rooney

Klabu ya soka ya Manchestr United yenye makao yake makuu jijini Old Traford nchini Uingereza imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kusalia na Wayne Rooney na kusema kamwe hawatofanya maamuzi ya haraka juu ya uhamisho wala uuzwaji wa mshambuliaji huyo.

Matangazo ya kibiashara

Akiwa ziarani jijini Hong Kong, mkongwe wa klabu hiyo Bobby Charlton amesema Rooney ni mchezaji wao na wataendelea kuwa naye kutokana na kuwa ni kipaji bora kwenye mchezo wa soka.

Kutokana na kukabiliwa na majeraha Rooney hajaandamana na wenzake ziarani barani Asia na Australia lakini Meneja wa United David Moyes amesema mchezaji huyo atakuwa sawa na kurejea kikosini hivi punde kwa ajili ya kushiriki mechi zijazo.

Charlton anayeshikilia rekodi ya kufunga magoli mengi zaidi katika historia ya klabu hiyo amesema anatumaini Rooney ana kipaji cha soka na ipo siku atavunja rekodi yake.

Kwa sasa Rooney ana jumla ya mabao 197 akiwa amebakiza mabao 52 pekee ili avunje rekodi ya Charlton.