JUDO

Rais wa Judo nchini Japan kujiuzulu baada ya uongozi wake kukumbwa na kashfa za ufisadi na udhalilishaji

lespritdujudo.com

Rais wa Shirikisho la Judo nchini Japan AJJF, Haruki Uemura atalazimika kuachia wadhifa wake mwezi ujao kutokana na uongozi wake kukabiliwa na kashfa za udhalilishaji wa wanawake na matumizi mabaya ya fedha.

Matangazo ya kibiashara

Uemura amewaambia waandishi wa habari kuwa atajiuzulu mwezi ujao sambamba wa wajumbe wengine wanne wa Shirikisho hilo walioweka bayana lengo lao la kuachia ngazi.

Shirika la habari la Kyodo limeripoti kuwa wanachama 15 wa zamani na wa sasa katika timu ya wanawake walisilisha malalamiko yao kwa kamati ya olimpiki ya nchi hiyo JOC wakilalamikia unyanyasaji waliokumbana nao toka kwa kocha Ryuji Sonoda na Maofisa wengine wa mchezo huo.

Wachezaji wa timu ya wanawake waliripoti kudhalilishwa kwa kuchapwa viboko na makofi wakati wa maandalizi ya michuano ya olimpiki ya mwaka jana. Ryuji alijiuzulu mwezi Januari ili kupisha uchunguzi huo kabla ya kamati ya olimpiki ya nchi hiyo kutangaza kusitisha ufadhili kwa AJJF.

Serikali ya Japan na Shirikisho la kimataifa la mchezo wa Judo IJC, wameitaka AJJF kujisafisha kutokana na shutuma zinazozidi kuelekezwa kwake.