michezo

Azarenka asheherekea siku ya kuzaliwa sambamba na ushindi

Bingwa wa Tennis kwa upande wa kinadada Victoria Azarenka asheherekea siku ya kuzaliwa kwa ushindi
Bingwa wa Tennis kwa upande wa kinadada Victoria Azarenka asheherekea siku ya kuzaliwa kwa ushindi REUTERS/Ben Solomon/Pool

Mwana dada Bingwa katika Tenis Victoria Azarenka,ambaye amcheza kwa mara ya kwanza tangu jeraha kumuondoa katika michuano ya Wimbledon amesheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kupata ushindi katika michuano ya wazi ya Southern Califonia huko Carlsbad siku ya jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Bingwa huyo wa michuano ya wazi ya Australia zarenka, akiwa na ubingwa nambari tatu ulimwenguni ameibuka katika robo fainali kwa ushindi wa seti 6-2, 6-3 katika mzunguko wa pili dhidi ya Bingwa wa zamani wa michuano ya wazi ya Ufaransa Francesca Schiavone huko Italia.

Akiwa mwenye furaha isiyo kifani ameeleza kupata faraja sana kwa ushindi huo hususan katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza miaka 24.

Mchezaji huyo hakucheza mchuano mwingine tangu alipojeruhiwa goti aliposhiriki Wimbledon katika mzunguko wa kwanza na kuibuka dhidi ya raia wa Ureno Maria Joao Koehler