Michezo

Raisi wa zamani wa shirikisho la kandanda nchini Benin atiwa nguvuni

Raisi wa shirikisho la kandanda nchini Benin Anjorin Moucharafou
Raisi wa shirikisho la kandanda nchini Benin Anjorin Moucharafou www.beninfootball.com

Raisi wa zamani wa Shirikisho la kandanda nchini Benin Anjorin Moucharafou ametiwa nguvuni kwa mara nyingine kwa siku mbili baada ya kushindwa kuongoza kwa muhula wa tatu.

Matangazo ya kibiashara

Moucharafou, alifikishwa mbele ya mahakama mnamo mwezi juali 2011 kwa matumizi mabaya ya fedha za shirikisho hilo ambapo aliwekwa chini ya ulinzi katika gereza la Cotonou ambapo juma hili aliitwa sambamba na muhasibu wa shirikisho hilo kwa mashtaka hayo.

Mfanyabiahsara huyo anatuhumiwa kuhusika na matumizi mabaya ya fedha takribani dola za kimarekani 650 kutoka kwa kampuni ya simu kati ya mwaka 2008 na 2010.

Moucharafou,ambaye alifurahia msaada wa Fifa na Caf Wakati shirikisho la soka nchini FA Benin lilipogawanyika katika pande mbili aliamua kutogombea nafasi hiyo kwa awa,mu ya tatu kupisha fursa ya amani katika kandanda la nchini humo.