RIADHA

Bolt apania kurejesha ubingwa wa dunia wa mbio za mita 100

Nyota wa mbio fupi wa Jamaica Usain Bolt
Nyota wa mbio fupi wa Jamaica Usain Bolt RFI

Nyota wa mbio fupi wa Jamaica Usain Bolt ametangaza kuwa tayari katika jitihada zake za kutetea taji lake la mita 200 na kurejesha ubingwa wa mbio za mita 100 katika mashindano ya Dunia juma lijalo. 

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika tukio lililo wakutanisha wadhamini huko Gorky Park jana Jumapili Bolt,amesema kuwa kwa sasa anakwenda moja kwa moja katika mafunzo kwa ajili ya mashindano ya Agosti 10-18 kwenye Uwanja wa Luzhniki.

Bolt amesema ni muhimu kurejesha ubingwa wa taji hilo la mita 100 ambalo alilipoteza kwa mchezaji mwenza ambaye kwa sasa ni majeruhi Yohan Blake, baada ya kuanza vibaya huko Daegu Korea Kusini mwaka 2011