SOKA

Gervinho na Chamakah kuondoka Arsenal kabla ya msimu mpya

Mshambuliaji wa Arsenal Gervinho
Mshambuliaji wa Arsenal Gervinho mail.com

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa Gervinho na Marouane Chamakh kwa pamoja wataondoka kwenye klabu hiyo kabla ya kuanza kwa msimu mpya. 

Matangazo ya kibiashara

Gervinho mshambuliaji wa timu ya taifa ya Cote d'Ivoire ambaye aliigharimu Arsenal paundi milioni 11 wakati alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2011 akitokea katika klabu ya Lille na Chamakh ambaye alihamia klabu hiyo kwa mkopo akitokea Bordeaux mwaka 2010 wameshindwa kung'ara katika michuano ya kombe la Emirates.
Akizungumza baada ya timu yake kuichakaza Galatasaray kwa magoli 2-1 kwenye mtanange wa jana Jumapili,Wenger amesema kuwa Gervinho ana uelekeo mzuri wa kwenda klabu ya Serie A Roma na Chamakh huenda akaelekea Crystal Palace.

Serie A Roma itamlipa Gervinho kiasi cha pauni milioni 6.9 huku taarifa zikieleza kuwa mchakato wa Chamakah kuhamia Crystal Palace bado haujafikia makubaliano.

Arsenal imejaribu mara mbili kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez bila mafanikio na wamefanikiwa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Ufaransa Yaya Sanogo mwenye umri wa miaka 20 akitokea Auxerre.