TENNIS

Juan Martin Del Porto amchakaza Isner Citi Open

Mcheza tennis Juan Martin Del Porto
Mcheza tennis Juan Martin Del Porto topnews.in

Juan Martin Del Potro wa Argentina jana Jumapili ameshinda mchezo wa ufunguzi baina yake na Mmarekani John Isner kwa seti 3-6, 6-1, na 6-2 mjini Washington na kushinda dola milioni 1.3 katika Citi Open, na kudhihirisha kuwa tishio kubwa kwenye michuano ijayo ya US Open. 

Matangazo ya kibiashara

Del Potro, akicheza kwa mara ya kwanza tangu kupoteza mchezo kwa Novak Djokovic katika nusu fainali ya mashindano ya Wimbledon mwezi uliopita, alionesha kiwango bora cha mchezo akijitengenezea nafasi nne za ushindi kati ya sita kabla ya mapumziko.

Baada ya kuonekana amechoka katika seti ya kwanza, Del Potro alicheza kwa uangalifu ili asifanye makosa karibu kipindi chote cha mchezo kilicho salia ili kumshinda Isner ambaye alishinda katika mashindano ya Atlanta wiki iliyopita na alikuwa akisaka taji la tatu kwa mwaka huu.