michezo

Florian Mayer amwondosha nje ya Kombe la Rogers mchezaji tegemeo wa Australia Bernard Tomic

Mcheza teniss wa Ujerumani Florian Mayer
Mcheza teniss wa Ujerumani Florian Mayer blogs.bettor.com

Mjerumani Florian Mayer amemwondosha nje ya Kombe la Rogers mchezaji tegemeo wa Australia Bernard Tomic katika mpambano uliopigwa huko Montreal jana Jumatatu, wakati Janko Tipsarevic akiendelea kukumbwa na huzuni ya matokeo baada ya kuondolewa katika raundi ya kwanza. 

Matangazo ya kibiashara

Mayer, anayekamata nafasi ya 50 duniani,ameibuka kutoka chini na kushinda kwa seti tatu za 5-7 6-3 6-3 wakati huu makala ya sita ya wachezaji wa kulipwa wa tenesi ikitimua vumbi katika anga la bluu na hali ya joto.

Tomic alivumilia kipindi kigumu miezi michache tangu shirikisho la wachezaji wa kulipwa duniani ATP kumfungia baba yake na kocha John kwa madai ya kumshambulia mfanya mazoezi mwenzake mnamo mwezi Mei.

Alianza vizuri jana Jumatatu lakini Mayer alitumia kosa alilofanya Bernad mwanzoni mwa seti ya pili na kumfanya ashinde.
Mayer mwenye umri wa miaka 29 akicheza mechi ngumu kwa mara ya kwanza tangu mwezi Machi, alihitaji alama moja tu kusawazisha mchezo kabla ya kurudia ushindi.