KENYA

Homeboyz haitashuka daraja asema Simiyu

Baadhi ya wachezaji wa timu ya  Homeboyz ya  Kakamega Kenya
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Homeboyz ya Kakamega Kenya futaa.com

Mshambuliaji wa timu ya Homeboyz ya Kakamega nchini Kenya Geoffrey Simiyu amesema ana imani kuwa timu itatetea taji lake kama mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya mwisho mwa msimu. 

Matangazo ya kibiashara

Homeboyz wako katika hatari ya kushuka chini, kutokana na kwamba wamekuwa katika nafasi ya kushuka daraja kwa muda zaidi hivi sasa.

Licha ya ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya SoNy Sugar wiki chache zilizopita, Homeboyz wameshindwa kupata uwezo mzuri na inaonekana kuongeza uwezekano wa kutengwa katika timu mbili zilizo chini.

Simiyu, ambaye alihamia klabu hiyo kutoka Muhoroni Youth katikati ya msimu ana kibarua cha kufunga mabao ambayo yataiweka Homeboyz mahali salama.

Aidha Simiyu anakiri kwamba wakati walionao ni mgumu lakini anatumaini kwamba timu yake inaweza kujiondoa katika hatari hiyo kutokana na kwamba kocha wao anafanya kazi kwa bidii sambamba na mmiliki wa klabu hiyo ambaye anawaunga mkono kwa namna anavyoweza hivyo nao watafanya kila wawezalo kuhakikisha wanashiriki ligi msimu ujao.