SOKA-ULAYA

Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Franck Ribery kuwania taji la mchezaji bora barani Ulaya

Nyota wa soka barani Ulaya Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Franck Ribery
Nyota wa soka barani Ulaya Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Franck Ribery ciyaaro.com

Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Franck Ribery watawania taji la mchezaji bora barani Ulaya wakati waandishi wa habari barani kote watakupiga kura zao Agosti 29 jijini Monaco, shirikisho la soka barani Ulaya UEFA imebainisha. 

Matangazo ya kibiashara

Wachezaji hao watatu waliibuka katika orodha hiyo baada ya awamu ya pili ya kura za awali kupigwa na kupunguza orodha imara ya wachezaji kumi.

Rais wa UEFA Michel Platini alianza mpango huo miaka miwili iliyopita kwa kushirikiana na kundi la vyombo vya habari vya michezo vya Ulaya (ESM) ambapo Messi na mchezaji mwenzake wa Barcelona Andres Iniesta kushinda tuzo katika vipindi viwili vya kwanza vya mchakato huo.