MADRID-CHELSEA

Mourinho: Licha ya kufungwa kimekuwa kipimo bora kwa timu yangu

Christian Ronaldo, Real Madrid winger
Christian Ronaldo, Real Madrid winger Reuters

Kufuatia kushuhudia timu yake ikilala kwa mabao 3-1 dhidi ya klabu yake ya zamani, kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amesema kuwa walistahili kufungwa kutokana na makosa ambayo waliyafanya.

Matangazo ya kibiashara

Klabu ya Chelsea ambayo sasa inanolewa na kocha huyo mwenye tambo nyingi ilikuwa na kibarua dhidi ya Real Madrid ya Uhispani ambayo iliwahi kufundishwa na Mourinho.

Timu hizo zilikutana kwenye fainali ya kimataifa ya mchezo wa kirafiki mjini Miami, Flordia nchini Marekani na kushuhudia jahazi la Chelsea likizama kwa kukubali kichapo cha mabao 3-1.

Mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Real Madrid Christiano Ronaldo ndie aliyekuwa mwiba kwa kocha wake wa zamani, baada ya kuiandikishia timu yake mabao 2 katika kila kipindi huku lile la chelsea la kufutia machozi likifungwa na Ramires.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya kushuhudia timu yake ikifungwa, kocha Jose Mourinho amesema kuwa licha ya kupoteza mchezo huo lakini wanaimani ulikuwa ni kipimo tosha kwao kujiandaa na ufungizi wa pazia la ligi kuu ya Uingereza itakayoanza mwezi huu.

Kocha wa Real Madrid, Carlo Anceloti amesema kuwa amefurahishwa na ushindi huo na kwamba ulikuwa ni moja kati ya michezo muhimu ambayo timu yake imecheza toka achukue kibarua cha kuinoa timu hiyo mwezi mmoja uliopita.