RIADHA

Edna Kiplagat atetea taji lake mashindano ya dunia jijini Moscow Urusi

in2eastafrica.net

Mwanariadha wa Kenya na bingwa wa mbio za nyika Edna Kiplagat, amefanikiwa kutetea ushindi wake baada ya kumaliza wa kwanza katika mashindano ya dunia yaliyofunguliwa rasmi leo Jumamosi jijini Moscow Urusi. 

Matangazo ya kibiashara

Edna mwenye umri wa miaka 33 ambaye mwaka uliopita alishika nafasi ya 20 katika mashindano ya Olympic, amemaliza mbio hizo kwa saa 2:25:44 mbele Valeria Straneo raia wa Italia ambaye ameongoza mbio hizo kwa muda mrefu hii leo na hatimaye kumaliza wa pili saa 2:25:58 huku mjapani Kayoko Fukushi akikamata nafasi ya tatu kwa kumaliza muda wa saa 2:27:45.

Bingwa wa mashindano ya Olympiki Tiki Gelana wa Ethiopia hakuweza kushiriki mashindano ya hii leo baada ya kuondolewa katika mashindano ya jijini London

Pazia la mashindano ya dunia ya riadha limefinguliwa mapema hii leo jijini Moscow nchini Urusi ambapo mbio za mita 100 na mita 400 kwa upande wa wanaume zimekimbiwa hii leo huku mbio za nyika kwa upande wa wanaume zikitaraji kuanza baadye leo.