UINGEREZA

Kocha wa Timu ya Taifa ya Uingereza, Roy Hodgson atathimini mustakabali wa Wyne Rooney

Mshambuliaji wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Uingereza, Wyne Rooney
Mshambuliaji wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Uingereza, Wyne Rooney REUTERS/Giampiero Sposito

Mshambuliaji wa Timu ya taifa ya Uingereza Wyne Rooney ameelezwa na Meneja wa Timu ya Taifa hilo Roy Hodgson kuwa ni sehemu muhimu ya kikosi hicho

Matangazo ya kibiashara

Mustakabali wa Rooney ndani ya kikosi cha manchester United bado una utata, hasa baada ya Timu ya Chelsea kuonesha nia ya kumchukua mchezaji huyo.
 

Hodgson amesema kuwa angependa kuona mustakabali wa Rooney ukiamuliwa, hata kama Meneja wa kikosi cha Manchester United David Moyes kusisitiza kuwa mchezaji huyo hatauzwa.
 

Hodgson amesema kwa upande wake anamthamini Rooney kuwa mchezaji wa Timu ya Taifa ya Uingereza kwa kuwa ni mmoja kati ya Wachezaji bora.
 

Mbali na Taarifa juu ya nia ya kuondoka Manchester United, Rooney amekuwa akipambana na jeraha alilolipata ambalo lilimfanya kukaa nje ya ziara ya michezo iliyofanyika Barani Asia.
 

Rooney ameonekana na kikosi cha Uingereza katika uwanja wa St George katikati mwa Uingereza siku ya leo asubuhi na Kocha Hodgson amesema kuwa amefanya vizuri kama ilivyokuwa ikitarajiwa.