Michuano ya Riadha ya Dunia-Urusi

Michuano ya Riadha ya dunia nchini Urusi yakosa msisimko

Mwanariadha wa zamani na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Riadha nchini Urusi, Tatyana Lebedeva
Mwanariadha wa zamani na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Riadha nchini Urusi, Tatyana Lebedeva

Mamlaka nchini Urusi imekabiliwa na Changamoto kubwa hii leo baada ya Mashabiki wa Michezo kutohudhuria kwa wingi michuano ya riadha ya Dunia jijini Moscow ambayo yamekuwa yakifanyika huku viti vikiwa vitupu bila wafuatiliaji wa mashindano hayo.

Matangazo ya kibiashara

Wakimbiaji mashuhuri duniani, bingwa wa mbio za mita 10,000 Mo Farah na Mruka viunzi wa Marekani Aries Merritt wameeleza kutoridhishwa na namna ambavyo watu wamejitokeza kushuhudia michuano hiyo katika uwanja wa Luzhniki wenye uwezo wa kubeba watu 84,745.
 

Michuano iliyofanyika asubuhi ilishuhudiwa huku viti vingi vikiwa vitupu, hata wakati wachezaji maarufu kama Usain Bolt ambaye alishindana mbio za mita 100 jumapili usiku, alijikuta akishuhudiwa na watu wachache huku viti vingi vikiwa vitupu.
 

Uwenyeji wa michuano hii nchini urusi ni jaribio kwa uwezo wa nchi hiyo kuandaa mashindano mbalimbali ya kimichezo ambapo Rais Vladmir Putin alipata kwa ajili ya miaka ijayo ambapo itashirikisha michuano ya Olimpiki ya majira ya Baridi mwaka 2014, sambamba na michuano ya mpira wa miguu ya kombe la dunia mwaka 2018.
 

Makamu wa Rais wa shirikisho la riadha nchini Urusi, Tatyana Lebedeva amekiri kuwa mashindano haya yamekumbwa na Changamoto ya kukosa watazamaji wa kutosha na kuwa viti vingi vilikuwa vitupu.
 

Mkuu huyo amekiri kuwa Tiketi nyingi zimegawiwa bure lakini amejitetea kuwa hawana uzoefu wa kuandaa michuano mikubwa ya riadha na kuwa bado kuna mambo mengi hawayafahamu.