Michuano ya Riadha ya Dunia-Urusi

Mo Farah afanikiwa kutinga Fainali za michuano ya riadha mita 5,000

Mwanariadha mwenye asili ya Kenya anayeiwakilisha uingereza katika mashindano ya Riadha ya dunia
Mwanariadha mwenye asili ya Kenya anayeiwakilisha uingereza katika mashindano ya Riadha ya dunia Reuters

Mo Farah ameendelea kuweka matumaini ya kushinda medali ya dhahabu kwa mbio za mita 10,000 na mita 5,000 baada ya kuingia fainali katika mashindano ya mbio fupi.

Matangazo ya kibiashara

Aliyekuwa akitetea ubingwa huo alishika nafasi ya tano akiwa amekimbia kwa dakika 13 na sekunde 23.93 nafasi ambayo ni ya mwisho kwa idadi ya wakimbiaji wanaotakiwa kuingia fainali.

Ikiwa Mwanariadha huyu mwenye asili ya kenya anayeiwakilisha Uingereza, atashinda mchuano wa Fainali utakaofanyika siku ya ijumaa atakuwa amemfikia Mwanariadha Raia wa Ethiopia Kenenisa Bekele na kuwa Mwanariadha wa pili Kwa kushinda medali ya dhahabu kwa mbio za mita 10,000 na mita 5,000 kwenye michuano hiyo.

Farah mwenye umri wa miaka 30 ambaye pia alifanya vizuri kwenye michuano ya Olimpiki ya jijini London amekuwa Raia wa kwanza wa Uingereza kushinda taji kwa mbio za mita 10,000 jumamosi juma lililopita na pia kufanikiwa kupata nafasi ya kutetea ubingwa wake aliojitwalia huko Daegu mwaka 2011.