UINGEREZA

Westham yatiliana saini na Stewart Downing kutoka Liverpool

Aliyekuwa Mchezaji wa Livepool, Stewart Downing aliyejiunga na kikosi cha West ham
Aliyekuwa Mchezaji wa Livepool, Stewart Downing aliyejiunga na kikosi cha West ham

Westham united hii leo imetangaza kumsajili mchezaji kutoka liverpool winga Stewart Downing kwa kiwango ambacho bado hakijafahamika.

Matangazo ya kibiashara

Downing, 29, ametia saini mkataba wa miaka minne na klabu ya mashariki mwa london mchezaji huyo akimfuata Mshambuliaji Andy Carroll aliyetoka Liverpool kuelekea Upton Park.
 

Downing amekiri kufurahishwa na hatua hiyo akisema kuwa ni fursa ya kipekee kuichezea Westham United na kuwa yu tayari kukitumikia kibarua chake kwenye mchezo wake wa kwanza ambao utakutanisha Klabu yake mpya na Cardiff City kipute kitakachopigwa siku ya jumamosi.
 

Downing ni mchazaji wa tano kusajiliwa na Meneja wa West Ham, Sam Allardyce akitanguliwa na Carroll, Razvan Rat, Mlinda mlango wa kihipsnia Adran na kiungo wa kati, Danny Whitehead.
 

Carrollalijiunga na Liverpool kwa kitita cha Pauni milioni 35 na Downing walijiunga na Liverpool kwa kitita cha pauni milioni 20 akitokea Aston Villa.
 

Carroll amekaribisha kuwasili kwa Downing ndani ya West Ham, ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter akipongeza usajili huo.