Urusi

Mashindano ya riadha ya dunia kuwakutanisha wakimbiaji maarufu jioni ya leo

Mkimbiaji na bingwa wa mbio za riadha wa dunia Ezekiel Kemboi
Mkimbiaji na bingwa wa mbio za riadha wa dunia Ezekiel Kemboi REUTERS/Lucy Nicholson

Leo ni siku ya sita ya mashindano ya riadha ya dunia yanayoendelea mjini Moscow nchini Urusi. 

Matangazo ya kibiashara

Mbio kadhaa zinakimbiwa jioni hii huku wakenya wakitarajiwa kutamba katika mbio za mita elfu tatu kuruka maji na viunzi kwa upande wa wanaume ,mbio ambazo wamekuwa wakitawala kwa kipindi kirefu.

Mkenya Ezekiel Kemboi ambaye ni bingwa wa dunia na Olimpiki atawaongoza wenzake Paul Kipsele Koech, Abel Kiprop Mutao na Benkamin Kiplagat kutafuta medali ya dhahabu mbizo ambazo pia zitashuhudiwa na rais Uhuru Kenyatta ambaye yuko ziarani nchini Urusi.

Hata hivyo, wakenya wanatarajiwa kupata ushindani mkali kutoka kwa Mfaransa Mahiedine Meklhisis Benabbad ambaye alinyakua medali ya fedha katika mashindano ya Olimpiki jijini London mwaka uliopita, pamoja na Mganda Benjamin Kiplagat.

Mbio zingine ambazo pia zitakuwa zinaangaziwa barani Afrika ni mbio za mita 1500 kwa upande wa wanawake ambapo ushindnai mkali uanatarjiwa kuwa kati ya wakenya na Waethiopia, wakiongozwa na Nancy Jebt Langat, Hellen Obiri na Faith Kipyegon.

Wanariadha wengine wa kuangaliwa katika mbio hizi ni Genzebe Dibaba wa Ethiopia, Jinefer Simpson wa Marekani na Abeba Aregawi wa Sweden.

Hadi sasa , Marekani wanaongoza kwa Medali 10, wakifuatwa na Urusi ,medali 7, Kenya na Ujerumani zipo katika nafasi ya tatu kwa medali 5, huku Ethiopia pia ikiwa na Medali 5.