UINGEREZA

Wyne Rooney kufanyiwa tathimini kabla ya kukutana na Swansea siku ya Jumamosi

Mshambuliaji wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Uingereza, Wyne Rooney
Mshambuliaji wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Uingereza, Wyne Rooney REUTERS/Giampiero Sposito

Meneja wa Timu ya Manchester United amesema kuwa atatathimini hali ya afya ya Mshambualiaji, Wayne Rooney kabla ya kuamua kama atamchezesha mchezaji huyo katika mchezo wa kwanza wa Manchester katika ufunguzi wa michuano ya Ligi kuu nchini Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Moyes atakiongoza Kikosi hicho kwa mara ya kwanza siku ya jumamosi mwishoni mwa juma hili ambapo Mabingwa hao watetezi watakutana na Swansea.

Rooney ambae amekuwa akitajwa sana juu ya mustakabali wake na nia ya Chelsea kumchukua mchezaji huyu, alikosa mechi kadhaa kutokana na maumivu ya bega na nyama za Paja.
 

Rooney alicheza kwa dakika 66 wakati timu ya Taifa ya uingereza ilipokutana na Scotland katika Mechi ya kirafiki siku ya jana katika uwanja wa Wembley.
 

Moyes amsema amshuhudia mchezo wa jana na kusema kuwa alicheza vizuri, hata hivyo amesema kuwa atatathimini maendeleo yake na kusisitiza kuwa hana mpango wa kumuuza mchezaji huyo.