LIGI KUU UINGEREZA

Kindumbwendumbwe leo katika ligi kuu Uingereza, Manchester City kuvaana na NewCastle United, Morinho bado anamatumini ya kumpata Rooney

Kocha mkuu wa Manchester City Emmanuel Pellegrini
Kocha mkuu wa Manchester City Emmanuel Pellegrini

Ligi kuu ya nchini Uingereza inaendelea leo ambapo mchuano wa hii leo kati ya Machester City na Newcastle United unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani. Kocha wa Man City Manuel Pellegrini naye amekuwa na haya ya kuzungumza saa chache kabla ya vijana wake kujitupa dimbani.

Matangazo ya kibiashara

Kocha Pellegrini amejigamba kuwa na timu bora na lengo la klabu yake ni kuhakikisha wanacheza michuano ya ligi ya mabingwa sio tu katika hatua ya makundi bali kuhakikisha wanapata ushindi kabisa. Kocha huyo ameendelea kuwa wanajiandaa kuhakikisha wanashinda timu zote ili kuhakikisha wanapata ushindi wa ligi kuu nchini Uingereza, staili ya mchezo wa soka ni tofauti tofauti huenda wakahitaji muda zaidi ili kuwawezesha wachezaji weke kucheza kama vile anavyohitaji.

Katika hatuwa nyingine kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema anaamini kwa sasa klabu yake ipo tayari kusonga mbele baada ya klabu hiyo kushuhudiwa katika mgawanyiko kwenye msimu uliopita, anachosisitiza kwa sasa ni ushirikiano utakaoiwezesha Chelsea kusonga mbele.

Mourinho aliyekabidhiwa mikoba ya kuinoa hiyo toka kwa aliyekuwa kocha wa mpito Raphael Benitez aliiwezesha The Blues kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya Hull City katika mechi ya ufunguzi iliyopigwa mwishoni mwa juma.

Mourinho anasema hajakata tamaa juu ya mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney kwani anatumai ipo siku atamjumlisha katika kikosi chake.