Football

Fenerbahce ya Uturuki kuikaribisha Arsenal ya Uingereza nyumbani jioni hii

Arsene Wenger Kocha mkuu wa Arsenal
Arsene Wenger Kocha mkuu wa Arsenal

Klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza inajitupa uwanjani jioni huu kumenyana na Fenerbahce ya Uturuki. Arsenal itakosa huduma ya kiungo wake wa kati Alex Oxlade-Chamberlain baada ya kupata jeraha la goti wakati wa mchuano wa ligi kuu nchini Uingereza siku ya Jumamosi iliyoita dhidi ya Aston Villa.

Matangazo ya kibiashara

Kocha Arsenal Wenger atawategemea mabeki kama Bacary Sagna, Kieran Gibbs na Nacho Monreal kushikilia ngome ya Arsenal watakapokuwa nchini uturuki leo hii.

Arsenal ina rekodi nzuri ya kufuzu katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kufanya hivyo kwa misimu 15 iliyopita.

Fenarbahce inashiriki katika michuano hii wakati ikisubiri matokeo ya rufaa waliowasilisha kwa shirikisho la soka barani Ulaya baada ya kufungiwa nje ya mashindano haya kwa kosa la kupanga matokeo.

Rufaa hiyo itaamuliwa tarehe 28 siku moja baada ya mchuano wa muaridano na Arsenal ugenini.