Football

Kocha wa timu ya taifa ya Nigeria ataja kikosi chake kitacho pambana na Malawi kuwania kufuzu kombe la dunia

Kocha wa timu ya taifa ya Nigeria Stephen Keshi
Kocha wa timu ya taifa ya Nigeria Stephen Keshi

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Nigeria Stephen Keshi amekitaja kikosi cha wachezaji 18 watakaomenyana na Malawi katika mchuano wa mwisho mwezi ujao mjini Calabar kutafuta tiketi ya kufuzu katika awamu ya mwisho ya kusaka nafasi ya kushiriki katika kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mara ya kwanza, Keshi amewajumuisha Nosa Igiebor anayesakata soka la kulipwa nchini Uhispania na Mshambulizi Emmanuel Emenike anayechezea klabu ya Fenerbahce ambaye atacheza kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa kombe la dunia mapema mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Nigeria watahitaji sare ili kufuzu katika hatua ya mwondoano lakini Malawi wanahitaji ushindi ili kusonga mbele.