Football-Arsenal

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger asema yupo tayari kumsajili Karim Benzama mshambuliaji wa Real Madrid

Arsene Wenger Kocha mkuu wa Arsenal
Arsene Wenger Kocha mkuu wa Arsenal

Klabu ya soka ya Arsenal kutoka nchini Uingereza ipo katika harakati za kuwasajili washambulizi wa klabu ya Real Madrid ya Uhispania Karim Benzema na Angel Di Maria.

Matangazo ya kibiashara

Gunners inasema iko tayari kutowa kitita cha Pauni Milioni 40 kumsajili Benzema, baada ya kumkosa Gonzalo Higuain na Luis Suarez wa Liverpool.

Baada ya ushindi wa mabao 3 kwa 0 dhidi ya Fernabache ya Uturuki katika mchuano wa kufuzu kwa awamu ya makundi ya klabu bingwa barani Ulaya, kocha Arsene Wenger amewaambia mashabiki wa klabu hiyo kuwa wasiwe na wasiwasi kwa sababu dirisha la usajili bado halijafungwa hadi tarehe 2 Septemba na mengi yatafanyika.

Ushindi huu umewaweka Arsenal  kwenye nafasi nzuri ya kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya hatua ya makundi.

Matoke ya mechi nyingine za kufuzu klabu bingwa ulaya, Dinamo Zagreb ilikubali kichapo cha bao 0 - 2 nyumbani kutoka kwa Austria Wien.

Ludogorets nayo imebwagizwa ma bao 2 - 4 na FC Basel ya Uswis, wakati Steaua Bucureşti ikitoshana nguvu  ya 1 - 1 na Legia Warszawa huku Schalke 04 ya ujerumani nayo ikashindwa kutamba nyumbani baada ya kutoka sare tasa ya 1 - 1 PAOK.