CHAN

Zambia, Zimbabwe, Angola, Msumbiji kumenyana kesho katika kuwania kufuzu michuano ya CHAN nchini Afrika Kusini

Timu ya taifa ya soka ya Zambia kesho Jumamosi watakuwa wenyeji wa Zimbabwe katika mchuano wa mzungumzo wa pili kufuzu katika michuano ya bara la Afrika baina ya wachezaji wanaocheza soka nyumbani CHAN nchini Afrika Kusini mwaka ujao.

Matangazo ya kibiashara

Mchuano huu utapigwa katika uwanja wa Kimataifa wa Levy Mwanawasa mjini Ndola, na ni mchuano muhimu kwa kocha wa Zambia Herve Renard baada ya kulazimishwa sare ya kutofungana jijini Harare mwishoni mwa juma lililopita.

Wachambuzi wa soka wanasema kuwa ikiwa Zambia watashindwa nyumbani kesho basi huenda kocha Renard akajiuzulu.

Mbali na mchuano huo wa kesho huko Zambia, Msumbiji watakuwa nyumbani kumenyana na Angola kabla ya kukutana katika mzungunguko wa pili mwishoni mwa mwezi huu.

Tayari timu kumi na nne zimefuzu katika michuano hiyo ya CHAN.